Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Kuna msanii mkubwa alinikataza kwenda WCB - Rich Mavoko
8 June 2016

Msanii Rich Mavoko ambaye sasa yupo chini ya Label ya WCB Wasafi amefunguka na kusema kuwa wakati tetesi za yeye kwenda kujiunga na label ya WCB Wasafi zimeenea kuna msanii mmoja mkubwa wa bongo fleva alimtumia ujumbe na kumwambia anaanzaje kwenda kusimamiwa kazi na msanii Diamond Platnum.
Rich Mavoko amesema hayo leo kwenye kipindi cha Planet Bongo na kudai kuwa msanii huyo alimuumiza sana kwa maneno yake hayo ila yeye ilibidi amjibu tu kuwa yeye hafamu ametoka wapi na anakwenda wapi hivyo hawezi kujua mipango ya Mungu kwenye safari yake ya muziki.
"Sijawahi kusema hili ila ukweli ni kwamba wakati nataka kwenda WCB kuna msanii mkubwa alinitumia ujumbe na kuniambia Rich Mavoko unakwendaje kusimamiwa kazi zako na Diamond Platnumz, kiukweli aliniumiza sana ila nilimjibu kwa roho moja kuwa brother wewe hujui mimi nimetoka wapi na nakwenda wapi hivyo huwezi kujua hata hili litakujae kwangu" alisema Rich Mavoko.
Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Brand new song
28 April
- So good EP release
28 April
- #NEW MUSIC #NEW artist #RAYMATS!
30 April




Leave your comment