TANZANIA: Country Boy ajisikia vibaya kutoelewana na Young Dee

 

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Country Boy amesema anajisikia vibaya kutoelewana na rapper Young Dee ambaye alikuwa rafiki yake wa karibu wa muda mrefu.

Wawili hao walipishana lugha wakati ambapo walikuwa wanatoa kazi mpya ya kundi la ‘Mtu Chee’ hali ambayo ilipelekea Young Dee kujitoa ndani ya kundi hilo ambalo lilikuwa likiundwa na Young Dee, Country na Stamina.

Akizungumza na Bongo5, Country Boy amesema kilichotokea kati yao, kimevuruga mambo mengi ambayo walikuwa wanafanya pamoja.

“Toka matatizo yatokee sijakaa na Young Dee, nammiss sana kwa sababu ni mshkaji ambaye namkubali sana, kila nikisikia sauti yake kuna vitu vizuri ndani yake naviona. Kwa hiyo ni rapper ambaye tunahitajiana sana,” alisema Country

Aliongeza,“Mimi nadhani muda ukifika ushkaji utarudi tena, kwenye maisha kuna kila kitu, migogoro na nini vyote ni sehemu ya maisha. Kwa hiyo mimi nadhani muda ukifika ushkaji utarudi tena,”

 

Chanzo: Bongo5

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment