TANZANIA: Hatuna tatizo na Nisher - Gnako

 

Mara baada ya Nisher kulalamika kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram na kusema kuwa video ya wimbo wa ‘Arosto’ aliufanya yeye na baadae Gnako kutoka wenye kundi la Weusi ambae ndiye mmiliki halali wa wimbo huo kuipotezea kuliiibua mtazamo tofauti hasa kwa mashabiki wa msanii huyo…

Director Nisher alilalamika na kusema kuwa video hiyo  ilimgharimu gharama za kiasi cha shilingi milioni 3.9 na Gnako kumpotezea pasipo kumlipa kitu chochote.

Akiongea na kipindi cha Super Mega cha Kings FM kinachoendeshwa na Divine Kweka, G-Nako alisema pamoja na Nisher kuwatupia lawama kibao Instagram, wao wamechagua kutojibizana kwakuwa hayo ni mambo ya kike.

Amedai kuwa makubaliano ya awali ya video hiyo hayakufanyika kwenye mtandao hivyo hawana haja ya kulumbana mtandaoni baada ya kupishana na muongozaji huyo.

Warawara amedai kuwa video aliyoongoza Hanscana ndiyo wanayoitambua kama official na tayari wameituma kwenye TV za nje ambako wanasubiri tu ianze kuchezwa.

Unaweza kusikiliza hapa mazungumzo ya Gnako kuhusiana na Nisher:

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment