Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Wema Sepetu aonyesha uzalendo kwa kumuombea kura Diamond
30 May 2016

Baada ya hivi karibuni Alikiba kuwaomba watanzania wampigie kura Diamond anayewania tuzo za BET, Wema Sepetu naye amefanya hivyo.
Wema ametumia mtandao wa Instagram kuwaambia mashabiki wake wampigie kura ex wake huyo aliyetajwa kuwania kipengele cha Best International Act: Africa.
“Uzalendo ndo unaotakiwa… Tanzania Kwanza Vingine Baadae… Ama nene…? Vote Vote Vote….,” ameandika Wema kwenye picha ya BET Awards aliyoiweka Instagram.
Mashabiki wengi wamempongeza kwa uzalendo huo aliounesha licha ya yeye na Diamond kuwa mbali kwa sasa kutokana na kila mmoja kuwa na maisha yake. Wema na mpenzi wa sasa wa Diamond kuwa na tofauti
Diamond anachuana na mastaa wengine wa Afrika wakiwemo Wizkid, Yemi Alade, AKA, Cassper Nyovest na wengine wawili.
Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Joe Chriss music
16 June
- Approval
16 June
- New sound dropping tonight
16 June
- Bleeding soul full lyrics
16 June




Leave your comment