TANZANIA: Kwa mahali nilipo sasa, nimepiga msamba maana siyo hatua za kawaida - Alikiba.

 

Msanii Alikiba amefunguka na kusema kwa mafanikio aliyopata toka amerudi kwenye muziki tena ndani ya muda ni mfupi ni sawa na kuchana msamba kwake maana siyo hatua za kawaida.

Alikiba alisema haya kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kusisitiza kuwa yeye kusaini mkataba na kampuni ya 'Sony Music' jambo kubwa sana katika maisha yake ya muziki.

"Kiukweli toka nimerudi rasmi kwenye game na kutoa wimbo wa Mwana mashabiki walipokea vizuri sana Africa Mashariki, na kadili nilivyokuja kutoa wimbo mwingine wa Chekecha walizidi kuongezeka mashabiki na kujiona nina mashabiki wengi, hivyo kuja kusaini mkataba na 'Sony Music' ndani ya muda mfupi hivi kwangu mimi najiona ni kama nimepiga msamba maana siyo hatua za kawaida" alisema Alikiba.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

 

Leave your comment