TANZANIA: Sio kila mtu anauwezo wa kuandika nyimbo - Wakazi

 

Rapper Wakazi ametoa sababu kubwa ya baadhi ya wasanii kuandikiana nyimbo, kitendo ambacho kwenye muziki wa bogo fleva bado ni ni changamoto.

Wakazi amesema wasanii huwa wanaandika nyimbo za wasanii wengine kwa sababu sio kila mtu ana uwezo au kipaji cha kuandika mashairi mazuri, na kufikisha ujumbe mzuri kwa jamii.

“Sio kila mtu anauwezo wa kuandika nyimbo, au kusema kwamba a good song writer, ujue kuna watu wana mkono mzuri ambao yeye akiandika mashairi yanamgusa mtu kwa haraka zaidi, na ujumbe unaweza ukakubalika na asilimia kubwa ya watu wanaokusikiliza kwa haraka, na mapema ukawa na impact na jamii nzima”, alisema Wakazi.

Wakazi ambaye ni rapper anayewania tuzo za KORA mwaka huu, amesema yeye binafsi ni mwandishi mzuri wa mashairi, hivyo hamsumbui kwenye uandishi wa nyimbo zake.

“Mi naandika mashairi yangu mwenyewe na ni kwamba nikiandika mashairi yangu yanawagusa watu”, alisema Wakazi.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment