TANZANIA: Hatuaangalii ukubwa wa jina la msanii, tunachokiangalia ni radha ya msanii - Mafikizolo

 

 

Kundi la muziki kutoka South Afrika Mafikizolo wamesema kolabo inaweza kumyanyua mtu katika muziki na kufanya akawa na nafasi nzuri kimataifa kwa hiyo kolabo ni kitu kizuri kwa wasanii.

Wakizungumza na Enewz Mafikizolo wamesema kuwa kwa wasanii wanaohitaji kolabo na kundi lao wao hawaangalii ukubwa wa jina la msanii bali wanachokiangalia radha ya msanii na uwezo wa mtu katika kuimba.

“Huwa hatuangalii jina la msanii sisi tukipenda tu radha ya msanii tunafanya nae kolabo na hivyo ndivyo wasanii wengine wanapaswa kuviangalia”, walisema Mafikizolo.

Huku wakitolea mfano walivyowapa nafasi uhuru na Maphorisa na kuwaweka juu katika ramani ya muziki wakati walikuwa hawatambuliki katika game ya muziki lakini wao waliweza kuwafanya wao kutambulika na wengine kuanza kuomba kolabo kwao.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment