TANZANIA: Diamond ndani ya ukumbi wa Barclays Center ifikapo July

 

Ni ukumbi wa ndani kwa ndani maarufu mno jijini New York, Marekani nyumbani kwa wasanii wakubwa wakiwemo Jay Z, Beyonce, Justin Bieber, Rihanna, Drake, taja kila msanii mkubwa wa Marekani, amewahi kutumbuiza hapo.

Na sasa Diamond, Wizkid na Flavour, watakuwa wasanii wa kwanza wanaofanyia muziki Afrika kuwahi kutumbuiza kwenye ukumbi huo. Mastaa hao watatumbuiza kwenye tamasha la muziki la One Africa July 22, 2016 kwenye ukumbi huo wenye uwezo wa kujaza watu 20,000.

 

Justin Bieber akitumbuiza kwenye ukumbi wa Barclays Center

 

“We are about to Make a History America!!!…. Platnumz Diamond with my Fellow African brothers and Sisters will be Shutting the Barclays Center Down! On the 22nd Jully 2016 in New York!…. 20k Seat Capacity!…Now make sure you tell your Friend to tell a Friend,” ameandika Diamond.

 

Beyonce na Jay Z wakitumbuiza kwenye ukumbi huo

 

Barclays Center ni ukumbi unaotumika kwa shughuli mbalimbali na upo Brooklyn, New York City. Pia hutumika kama uwanja wa nyumbani wa timu ya kikapu ya Brooklyn Nets pamoja na New York Islanders ya National Hockey League.

 

Rihanna ndani ya Barclays Center

 

Show ya kwanza kufanyika kwenye ukumbi huo ilikuwa ya Jay Z, September 28, 2012.

 

Chanzo: Bongo5

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment