TANZANIA: Nahreel aongelea swala la maprodyuza kuwafanyia fear wasanii
10 May 2016

Msanii na prodyuza wa studio ya The Industry Nahreel amesema kwamba ni kweli kuwa wasanii wengi huwa wanafanyiwa fear sana na maprodyuza.
“Ni kweli kwamba maprodyuza wengi wanawafanyia fear wasanii, it’s true.. Kuanzia kwenye kurekodi mpaka inapofikia kwenye malipo. Mimi mwenyewe sijafaidika sana na muziki nikiwa kama prodyuza. Tunapewa tu hela flani ambayo tunajisongesha lakini kiukweli hailipi. Lakini inatokana na ufahamu na kutokuthamini au ni utamaduni tu mabao upo katika utamaduni wetu wa muziki hapa nchini”
Mbali na hayo msanii huyo ambaye anaunda kundi la NavyKenzo hivi karibuni aliwatambulisha wasanii wa lebo yake ya The Industry ambao ni Seline, Wildad pamoja na Rosa Ree.
Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz




Leave your comment