TANZANIA: The Industry yawatambulisha wasanii wake wa 3 kwa mpigo
9 May 2016

Kundi la Navy Kenzo kupitia studio yao iitwayo The Industry, kundi linaloundwa na Nahreel pamoja na Aika Marealle wamewatambulisha wasanii watatu kuingia katika label hiyo. Wasanii hao ni Rosa Ree, Seline pamoja na Wildad.
Hii hapa ni taarifa iliyotolewa na The Industry:
THE INDUSTRY MUSIC LABEL
TAARIFA KWA UMMA,
THE INDUSTRY YATAMBULISHA RASMI WASANII WAKE MBELE YA WAANDISHI WA HABARI
Kampuni ya Muziki ya The Industry iliyoko chini ya Producer wa Music Nahreel siku ya leo tarehe 6 mwezi wa Tano 2016 imewatambulisha wanamuziki wake watatu wapya ambao watakuwa chini ya usimamizi wa label hiyo.
Kati ya wasanii hao watatu wawili ni wake kike ambao ni Rosa Ree na Seline na Wakiume mmoja ajulikanae kwa jina la Wildad
The Industry wamesema kazi zao zitaanza kuchezwa redioni na kwenye TV siku si nyingi ambapo jumatatu ijayo wataachia wimbo wa Seline pamoja na Video yake
The Industry ni studio na kampuni ya muziki ambayo ipo chini ya kundi la music lenye Mafanikio makubwa la Navy Kenzo ikisimamiwa na Producer Nahreel na msaidizi wake Aika Marealle
Wasanii Baadhi Waliokwisha fanya kazi na Studio ya The Industry mpaka sasa toka kuanzishwa kwake hivi karibuni ni Diamond Platnumz na wimbo wake wa Nana, Nikki wa Pili na wimbo wa Baba Swalehe, Joh Makini na nyimbo zake kama Don’t Bother na nusu nusu.
Imetolewa na,
The Industry PR






Leave your comment