Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Shilole hujamzidi Vanessa kwa uzuri- Mashabiki
9 May 2016

Ikiwa zimepita siku kadhaa toka msanii Shilole afunguke kwenye kipindi cha 5Selekt kinachorushwa kwenye ting'a namba moja kwa vijana EATV kuwa hakuna msanii wa bongo fleva mzuri zaidi yake, mashabiki wameamua kutoa ya mioyoni.
Mashabiki wamemchana Shilole na kusema kuwa yeye si mwanamke mzuri katika wasanii wanaofanya bongo fleva huku wakisema kuwa uzuri wake hausofei kabisa kwa msanii Vanessa Mdee.
Baadhi ya mashabiki walikuwa wakimpa madongo kuwa mwanamke mzuri hawezi kujianika kama yeye, huku wengine wakisema kuwa mwanamke mzuri hawezi kuwa yeye kutokana na tabia yake ya kutojiheshimu na wengine wakisema kuwa yeye hana lolote na wa kawaida kabisa.
"Kuna manzi wakuitwa Vanessa cheki yule manzi alivyo mcute wewe nani wachakuji puraaaaaaaaaaa" Africanboihacker

Weekly Top 10 songs
Top stories
- Brand new song
28 April
- #NEW MUSIC #NEW artist #RAYMATS!
30 April
- Music artist Henz Davy Says
29 April




Leave your comment