Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Hakuna anayemuandikia mwenzake WCB, wanasaidiana tu – Ricardo Momo
4 May 2016

Baada ya fununu kuzagaa juu ya msanii anayetamba kutoka lebo ya Wasafi Raymond Tip Top kuwa ndiye msanii anayeibeba lebo hiyo meneja wake Ricardo Momo amefunguka juu ya fununu hizo.
Akikanusha fununu hizo Ricardo alisema kuwa si kweli kwakuwa kila msanii katika lebo yao huwa anajitungia nyimbo yeye mwenyewe "labda kusaidiana tu kimawazo".
“Hakuna anayemuandikia mwingine ila wanasaidizana wote kwa pamoja kila mtu ana uwezo wake na kila mtu anajiamini kwa kile anachokifanya”, alisema Ricardo.
Fununu zilizopo mitaani ni kuwa msanii Raymond ndiye muandishi wa nyimbo nyingi zadi katika lebo hiyo mpaka ngoma ya Bado iliyoimbwa na Harmonize ambayo alipokonywa na kupewa Harmonize.
Ricardo aliongeza kuwa awali wasanii hao wote nyimbo zao zilikuwa na jina moja la 'Bado' na wao wakaona haifai ndiyo wakaamua kutofautisha majina na kuita 'kwetu' na 'Bado'.
Weekly Top 10 songs
Top stories
- Brand new song
28 April
- #NEW MUSIC #NEW artist #RAYMATS!
30 April
- Music artist Henz Davy Says
29 April




Leave your comment