TANZANIA: Winess amlamba makofi msichana aliyetaka kuchepuka na mpenzi wake Ochu
29 April 2016

Star wa Bongofleva Witness anaetamba kwa jina jipya la Kibonge Mwepesi amedhihirisha kuwa yeye ni matata baada ya hivi karibuni kutembeza kichapo kwa dada mmoja mbele ya umati wa watu.
Akizungumza na Enewz Witness alisema kuwa alimlamba makofi dada huyo ambaye alikuwa anataka kuchepuka na mwandani wake baada ya kumletea dharau wakati yeye alipokuwa anania ya kumuonya tu.
“Unajua watoto wa Kiswahili wanakera sana na huyu ni mfano tuu kwa sababu kila ngoma mpya ya Ochu inapotoka tu watoto wakike wanaanza kumfuata fuata sasa jamani kwanini mnasubiria ngoma mpya tu ?, ” alihoji Witness.




Leave your comment