Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Wimbo wa 'Freedom' wazua utata kwa Mr Blue
27 April 2016

Msanii wa Bongefleva ambaye jina lake lilianza kushine kwenye game ya muziki wa Bongofleva toka akiwa na umri mdogo Mr. Blue, amerudi kwenye headlines baada ya kupost kupitia account yake ya instagram na kuelezea kwa hisia zake kuhusu wimbo mpya alioutoa Mr. II Sugu kuwa ni wimbo ambao alimshirikisha na anashangaa kuona mambo yapo tofauti.
Alipost na kusema:

"Ndugu zangu nipeni ushauri kwa hili niliona nikae kimya ila limeniuma sana kwa kweli ..!! SUGU namuheshimu km kaka yangu kimuziki na kiumri pia ..sasa kuna nyimbo nilimshirikisha inaitwa "Freedom" tulifanya pale kwa makochali na hiyo ndo picha ya ushahidi na nyimbo ipo youtube kwa wasioisikia..sasa kinachonishangaza leo kuona ameitoa verse yangu na kuweka verse zake mbili na kaishoot mpaka video na nyimbo imekuwa yake tena bila kunitaarifu mimi mwenyewe au ridhaa yoyote kutoka kwangu je hii ni haki kweli??? Maana mtu ukiongea unaonekana unatafuta kiki au sijui nn...mi imeniuma kwa kweli jamani je mnanishauri nini ndugu zangu....????"
Weekly Top 10 songs
Top stories
- #NEW MUSIC #NEW artist #RAYMATS!
30 April
- Music artist Henz Davy Says
29 April
- Music artist Henz Davy Says
29 April
- BABA FELA
30 April




Leave your comment