TANZANIA: Kuoa kwangu sio sababu ya kushuka kimuziki – Mr Blue

Msanii huyo ameyasema hayo katika kipindi cha eNEWS kinachorushwa na kituo cha Eatv ambapo mtangazaji alimuuliza kuhusiana na yeye kuoa na haoni kwamba anaweza kushuka katika kazi zake za sanaa.

"Mimi siwezi kufeli kwenye muziki nimepata mitihani mingi kwenye muziki lakini sijashuka hadi leo, nimeanza muziki nikiwa mtoto na sasa hivi nimeshapata mtoto bado nipo kwenye muziki".

''Muziki ni kazi wapo wasanii wengi wa Marekani wameoa lakini wanafanya vizuri, kwa Tanzania mfano Mzee Yusuf ameoa mara mbili lakini sio kwamba ameshuka kwenye game kwa hiyo habari hizi siyo za kweli kabisa''- Amesisitiza Mr. Blue.

Mr. Blue amefunga ndoa hivi karibuni jijini Dar es salaam ambapo kwa sasa ana watoto wawili.

 

Leave your comment