Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Video: Diamond aongea haya baada ya kifo cha Papa Wemba
25 April 2016

Wiki tatu kabla ya kifo cha Papa Wemba, Jumapili ya jana, Diamond alirekodi wimbo naye jijini Paris, Ufaransa.
Akiwa kwenye ziara yake ya Ulaya, Diamond alienda Paris na kuingia studio na msanii huyo kurekodi wimbo huo alioshirikishwa. Hakusema awali kwakuwa kilichobainika kwenye safari hiyo ni kuingia studio na Fally Ipupa aliyemshirikisha.
Diamond amepost videokupiti ukurasa wake wa Instagram inayowaonesha wawili hao wakiwa studio baada ya kurekodi wimbo. Wimbo huo unasikika kwenye video hiyo chini.
“Wiki nne tu zilizopita tulikuwa Paris, akanishirikisha kwenye nyimbo yake, tukapanga mengi juu ya wimbo halaf ghafla naskia habari ya Msiba…Dah! nimesikitika sana, Hakika binadamu ni wazungumzaji tu ila Mwenyez Mungu ndio Mpangaji…Pumzika salama Kiongozi wetu daima tutakukumbuka, #RipPapaWemba,” ameandika Diamond.
Papa Wemba alifariki Jumapili hii baada ya kuanguka jukwaani alipokuwa akitumbuiza kwenye tamasha kubwa nchini Ivory Coast.
Chanzo: Bongo5
Weekly Top 10 songs

Black Mark utandilubi omwami wangu5:21
KAPEKE LONDON2:23
In My Bed2:50
Paver2:55
CHAMPION GAL3:00
Ex Nkubilako ft DonMusa2:55
BIkola2:58
The Prelude of Grace1:31
Joy Is Coming3:08
Worship My King5:00


Leave your comment