Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Dudubaya asema hawezi kumuomba msamaha Chidi Benz
22 April 2016

Msanii mkongwe wa muziki, Dudu Baya, amesema hawezi muomba msamaha Chidi Benz kutokana na kauli yake ‘acha afe’ ambayo aliitoa baada ya rapa huyo kuzidiwa na matumizi ya Madawa ya kulevya na kuomba msaada. Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Dudu Baya amesema aliitoa kauli hiyo baada ya kuona rapa huyo hakuwa tayari kusaidiwa na watu ambao walijitokeza kumsaidia.
“Siwezi kumuomba msamaha Chidi Benz kwa kauli yangu ya acha afe,” alisema Dudu Baya “Nachoweza kufanya ni kumpa pole kwa matatizo yaliyompata, na ninamwombea dua Mungu ampe nguvu mpya, akili mpya, mwanga mpya. Bongofleva inamwitaji, jamii imemmis, familia yake inamwitaji na inamtegemea. My best rapper, my friend Chidi Benz hakuna wa kukuokoa, jiokoe,”
Chizi Benz kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kukubali kupelekwa Bagamoyo Sober House kumsaidiwa kuondokana na matatizo yanayomkabili.
Weekly Top 10 songs

Kamwambie3:47
chile-one-so-lucky4:02
Buwooma2:44
Joy Is Coming3:08
Nakupenda3:12
Udede Ft Msomali x Malume & Samas Alifata Hela Remix6:34
Msaliti 11:25
Paver2:55
Ssirivawo ft yven feiz2:10
Ziyakuba kabotu6:57
Top stories
- #NEW MUSIC #NEW artist #RAYMATS!
30 April
- Nordman--Kelly yo collabo
30 April
- One and only
01 May


Leave your comment