TANZANIA: Kauli ya Bright kumpenda Vanessa yavunja uhusiano wake na mpenzi wake

Baada ya Bright kuweka hadharani kuwa anampenda sana Vanessa Mdee na kuweka dwazi kwamba yuko tayari kumnyang’anya Jux ili aweze kumuoa yeye, mpenzi wa msanii ambaye jina lake halikujulikana, amesikika binti huyo akiongea kwa simu na Bright ambaye alirekodiwa bila kujua, na kutoa kauli kuwa hamuhitaji tena aende kwa huyo huyo Vanessa Mdee.


Binti huyo alisikika akisema kama hataki tena kuwa na mahusiano na msanii huyo ingawa bado anampenda, na kumtaka akamuoe Vanessa aliyemtaja kwenye media.


Bright ambaye ameachia wimbo wake wa 'Nitunzie' aliomshirikisha Baraka Da Prince, ambao pia ameu-dedicate kwa Vanessa Mdee, hapo jana alifanya interview na Planet Bongo, na kusema hadharani kuwa anampenda Vanessa Mdee, na yuko tayari kufanya chochote ili mradi amuoe awe mke wake rasmi.

Leave your comment