Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Khadija Kopa anampango wa kuanzisha bendi ya familia
15 April 2016

Gwiji la taarabu, Malkia Khadija Omary Kopa yupo kwenye mchakato wa kuanzisha bendi kwa ajili ya familia yake.
Akihojiwa na kipindi namba 1 cha burudani nchini (Enews) cha EATV ameeleza kuwa amechelewa kuanzisha bendi hiyo kwa sababu yeye ni mwajiriwa wa TOT na alikuwa na kazi nyingi sana.
Aidha alikuwa akifanya kazi kama bendi ingawa hakuwa na bendi, alikuwa anakodi wasanii anafanya nao kazi, anawalipa. Amesisitiza kuwa watoto wake sasa wamekuwa waimbaji hivyo hana budi kutengeneza bendi kwa ajili yao.
Ameongeza kuwa anafanya hivyo kwa sababu itafika kipindi yeye ataacha muziki na kufanya shughuli nyingine tofauti na muziki.
Mwimbaji huyo wa miondoko ya taarabu amesema kuwa bendi hiyo itajumuisha pia wasanii wa nje ila ameitengeneza kifamilia kwasababu amewatengenezea watoto wake.
Weekly Top 10 songs

Kamwambie3:47
chile-one-so-lucky4:02
Buwooma2:44
Joy Is Coming3:08
Nakupenda3:12
Udede Ft Msomali x Malume & Samas Alifata Hela Remix6:34
Msaliti 11:25
Paver2:55
Ssirivawo ft yven feiz2:10
Ziyakuba kabotu6:57
Top stories
- #NEW MUSIC #NEW artist #RAYMATS!
30 April
- One and only
01 May
- SHUKRANI
02 May


Leave your comment