TANZANIA: Nimeamua kusafiri na mama kumtoa ushamba!!! – Diamond Platnumz
14 April 2016

Msanii wa miondoko ya pop nchini Tanzania, Diamond Platnumz ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul anamesema aliamua kusafiri na mama yake mzazi katika tour aliyoipa jina la #From TanzdaleTo WorldTour. Diamond Platnumz alisafiri hivi karibuni akiwa na familia yake yote akiwemo mama yake mzazi, mpenzi wake Zari pamoja na mtoto wake Latifa Naseeb ‘Princess Tiffa’.
Msanii huyo amesema hii ni mara yake ya kwanza kusafiri na familia yake, kama mama yake hajawahi kwenda ulaya kabisa hivyo ameamua kumtoa ushamba."Miaka inaenda na tangia 'nimetoboa' sikuwahi kusafiri na mama yangu kwanza hakuwahi kwenda Europe au Ulaya alikuwa anaisikia tu kwenye bomba, inaweza kuwa kesho au kesho kutwa nikadondoka nikafa halafu mama yangu akabaki tena kuisikia nikaona ni bora kwenda kutoana ushamba kabisa"
Aidha msanii huyo amesema ataendelea na 'tour' yake ambapo atafanya 'show' 3 marekani, na pia 'show' nyingine zitafanyika India, Dar es Salaam , Mwanza, na Australia. Diamond ameongeza kuwa atakuwa na 'tour' rasmi kwa ajili ya Afrika na amesisitiza kuwa kuna nyimbo anasubiri zitoke maalum kwa ajili ya Afrika.




Leave your comment