Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Idris alisingiziwa mtoto
12 April 2016

Akizungumza kupitia kipindi cha 'Mkasi' kinachorushwa na EATV Idris Sultan alisema alivyoletewa mtoto alibaki akishangaa na alivyomwangalia vizuri yule mtoto aliona ni kama anafanana na msanii Diamond Platnumz kwanza kutokana na rangi yake na jinsi yule mtoto alivyo.
"Unajua siku nimerudi kutoka kwenye mashindano ya Big Brother nilisingiziwa kuwa nina watoto watatu, na mmoja alimleta mtoto mpaka nyumbani lakini nilivyomuangalia yule mtoto niliona kama anafanana na Diamond Platnumz kwanza ile rangi ya weusi na jinsi mtoto alivyo, nikaona isiwe taabu nikampigia simu Diamond Platnumz nikamwambia na yeye akaja kumuangalia yule mtoto lakini akasema na yeye si wake. Yule mama mtoto alikuwa anatokea Mtwara hivyo mpaka leo baba wa yule mtoto bado hajafahamika" alisema Idris Sultan
Mbali na hilo mchekeshaji huyo ameelezea namna ambavyo anaweza kuishi na marafiki zake wa karibu ambao kwa sasa wote hawaongea, akiwepo Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz na Wema Sepetu na ndipo aliposema yeye anaweza kwenda nao sawa.
"Unajua mimi ninapokuwa na Wema Sepetu ninazungumza naye mambo yangu mimi na yeye hivyo siwezi kuwa na yeye nianze kuzungumza mambo ya mtu mwingine na hiyo ndiyo njia inayofanya niweze kuishi nao pasipokuwa na tatizo, unajua hawa wote kwangu mimi ni muhimu sana mimi nawahitaji wao na sijui kama wao wanatambua hilo" alisisitiza Idris Sultan
Chanzo: Enewz
Weekly Top 10 songs

Kamwambie3:47
chile-one-so-lucky4:02
Buwooma2:44
Joy Is Coming3:08
Nakupenda3:12
Udede Ft Msomali x Malume & Samas Alifata Hela Remix6:34
Msaliti 11:25
Paver2:55
Ssirivawo ft yven feiz2:10
Ziyakuba kabotu6:57
Top stories
- One and only
01 May
- SHUKRANI
02 May
- Jaxon Ryker Official profile
30 April


Leave your comment