Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
TANZANIA: Jay Dee akutana na Ray C baada ya miaka 6
12 April 2016

Msanii wa bongo fleva ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa 'Ndi Ndi Ndi' Lady Jaydee amekutana na msanii Ray C baada ya miaka sita. Baada ya kuonana Lady Jaydee alisema kila mtu anapitia magumu katika maisha kwa njia tofauti. "Kila mtu anapitia magumu katika maisha kwa njia tofauti hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea, amini na amua nakupa moyo na Mungu akusaidie kwa yote unayopitia akuondolee akuepushie na akupe kufahamu na kukiri mabaya" aliandika Lady Jaydee
Lady Jaydee aliendelea kumtia moyo msanii huyo na kumwambia kuwa kwa sasa anakumbuka ule ushindani waliokuwa nao kipindi cha nyuma kwenye muziki na kumweleza kuwa arudi tena kwani bado ana nafasi ya kuweza kufanya vizuri. "Nakumbuka tulivyo anza kimtindo nai miss 'competition' tafadhali rudi tena naamini bado unayo nafasi. Binti amka jikaze anza mwendo umrembo na bado wang'ara. Ni baada ya miaka 6 tangu kuonana mara ya mwisho story nazo ni ndefu na nyingi". Aliandika Lady Jaydee

Chanzo: Enewz
Weekly Top 10 songs

Black Mark utandilubi omwami wangu5:21
KAPEKE LONDON2:23
In My Bed2:50
Paver2:55
CHAMPION GAL3:00
Ex Nkubilako ft DonMusa2:55
BIkola2:58
The Prelude of Grace1:31
Joy Is Coming3:08
Worship My King5:00


Leave your comment