TANZANIA: Diamond aja na reality show

 

Msanii anayefanya poa sana katika muziki wa bongofleva nchini Tanzania, Naseeb Abdul ak.a Diamond Platnumz anatarajia kutoa kipindi kitakachoonyesha maisha yake halisi anayoishi kila siku. Msanii huyo amedai kuwa reality show hiyo itaonyesha vituko, mikasa na matukio mbalimbali yanayomuhusu yeye na team yake nzima.
Katika mtandao wa Instagram msanii huyo alipost na kuandika:
(Can you try to guess the name of our Reality Show?) (Muda si Mwingi Kipindi cha Maisha yangu ya kila siku, Familia na Team yangu nzima itaanza kuwa kwa Tv yako pendwa... nakuahidi sio tu eti Kireality show:-)... ni Reality show Bora ambayo naamini utaipenda kunzia kwenye Quality, Mikasa na matukio yote nnayopitia mimi, Familia na Team yangu kila siku....Mengi yanaonekana, Unayoyasikia, Unayasoma ila kwenye Hiki kipindi ndio itakuwa Thibitisho la kila uvumi uusikiao....Sjui Kipini puani, Mara jicho, Mara sjui @officialshetta , Mara DNA, Mara @romyjons kutoinekana tena kwenye Tour Ghafla....Niamini mimi yote utaona na kuyapata kwa uwazi kabisa, Kaa na Mimi.......! We unavyohisi reality Show yetu itakuwa inaitwaje.....? Cc @zarithebosslady @romyjons #VodacomKaziNiKwako
Diamond ametoa nafasi kwa mashabiki wake kumtajia jina watakalo penda litumike kama jina la kipindi hicho.

Leave your comment