TANZANIA: Kipini cha Diamond cha washangaza mashabiki
8 April 2016

Supa Staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz ametupia picha kwenye akaunt yake ya Instagram akiwa ametobua Pua na kuweka kipini. Hata hivyo Hali sio nzuri juu ya Mashabiki wake wengine wakimponda na wengine wakimpongeza. Kinachowaumiza mashabiki ni kwamba haoneshi kujali kilio chao. Aliwashtua mashabiki wake baada ya kupost picha ikimuonesha ameweka kipini. “Bro hapo umezingua mimi nimekuwa shabiki wako tangu 2010 mpaka now nakubali kila ukifanyacho bt kwa hili nimeshusha vyeo cz tambua wew ni mtoto waa kiislam hapo ume feel bro nitaendelea kusapoti muziki wako ila tambua ila tambua umewakwaza wengi”, aliandika shabiki mmoja.
Baadaye tena alipost picha nyingine ambayo ilikua inamuonesha hana kipini kitendo kilichowafanya mashabiki wapumue, lakini baadae alituma video ikimuonyesha akiwa na kipini hicho. Ndipo shabiki mmoja alicomment na kusema “ Bro sorry bana tunaokuelewa ni wengi ila daah kwa hiyo ishu unatupambanisha na maadui maana tunakosa majibu , kama kuna uwezekano me nahisi fanya utoe”.




Leave your comment