TANZANIA: Mastaa wa Bongo wenye followers wengi Instagram
8 April 2016

Tunafahamu kuwa mtandao wa kijamii unaongoza duniani ni Facebookikiwa na wastani wa watumiaji milioni 7.5 ikifuatiwa na Twitter, ila kwa sasa tunalenga kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram. Mtandao wa Instagram nchini Tanzania umekua ni moja kati ya mitandao ya kijamii unaoweza kukusanya mashabiki wengi nchini. Wapo mastaa ambao wanaongoza kwa kuwa na followers wengi.

- Diamond Platnumz

Jina kamili anaitwa Naseeb Abdul, ni msanii wa muziki wa bongo fleva nchini. Ametoa nyimbo kama vile ‘Mdogo mdogo’, Utanipendaga na nyinginezo nyingi. Ndiye anayeongoza kwakuwa na mashabiki wengi instagramwenye idadi ya 2,060,462.

- Wema Sepetu

Wema Sepetu alikua ni Miss Tanzania mwaka 2006 na kujikita katika uigizaji. Wema Sepetu pia ni mmiliki wa lipstick za Kiss By Wema. Katika akaunti ake ya Instagram anamashabiki 1,604,968.

- Millard Ayo

Ni mtangazaji maarufu nchini ambaye pia anamiliki studio yake mwenyewe. Millard Ayo ambaye amejizolea umaarufu wa redioni na kwenye mitandao kwa kuwa na mashabiki 1,588,670.

- Jokate Mwegelo

Ni mwanamitindo na pia ni msanii. Alishawahi kushika nafasi ya tatu ya kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Tanzania mwaka 2006 na kushika nafasi ya 3. Jokate katika mtandao wa Instagram ana mashabiki 1,508,992.

- Jackline Wolper

Ni muigizaji maarufu nchini Tanzania amabye anafanya vizuri sana. Katika mtandao wa Instagram Jackline Wolper ana mashabiki 1,489,460.

- Vanessa Mdee

Ni mwanamuziki wa bongofleva nchini, ambaye awali alikua ni Mtangazaji wa Mtv na pia kuwa mtangazaji wa Times Fm Radio. Ila kwa sasa mrembo huyo amejikita katika muziki na kutoa nyimbo kama Niroge, Never Ever, Closer na nyinginezo nyingi. Katika mtandao wa Instagram Vanessa Mdee au Vee Money anamashabiki 1,409,179.

- Shilole

Ni staa wa muziki nchini pamoja na uigizaji. Msanii huyu alishawahi kutoa nyimbo kama vile Ana Malele, Namchukua, na nyinginezo nyingi. Katika mtandao wa instagram Shilole ana mashabiki 1,389,039

- Linah Sanga

Ni msanii wa muziki nchini aliyetoka katika nyumba ya vipaji THT ‘Tanzania House of Talent’. Ni mwanadada mwenye sauti ya kipekee. Katika mtandao wa Instagram Linah anamashabiki 1,175,426

- Alikiba

Ni msanii anayekubalika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Alishatoa nyimbo kama Chekecha , Cinderella na nyinginezo nyingi. Alikiba katika mtandao wa kijamii ana mashabiki 1,046,606

- Elizabeth Michael

Ni muigizaji anayefanya vizuri nchini Tanzania. Hivi karibuni alipata tuzo huko nchini Nigeria. Katika mtandao wa instagram, Elizabeth au Lulu ana mashabiki 1,041,886





Leave your comment