TANZANIA: Babutale aeleza mipango waliyonayo na Hakeem wa Empire.
6 April 2016

Diamond Pltnumz na meneja wake Babu Tale wanajitahidi kutumia kila fursa inayoajia mbele yao. Hivi karibuni wawili hao walikutana na mwigizaji maarufu wa Series ya ‘Empire’ Yazz anayejulikana Zaidi kama ‘Hakeem’ jijini Los Angels, Marekani.
Kupitia kipindi cha Playist cha Times Fm, Babutale alieliza jinsi walivyokutana na msanii huyo na kilichofuata baada ya hapo. “Jamaa ‘Yazz’ alikuja kwenye hoteli tuliofikia na alikuwa na mabo yake. Mimi sijuagi zile movie nisiwe muongo, nimemuona tu hivi akina Diamond anaongea nae. Mchana nimeona mabango yake mji mzima, LA nzima imechafua Billboard, kwahiyo nikamkumbuka huyu nimemuona mchana, baada ya kumuona kula niliporudi ilibidi niangalie Empire vizuri. Pale tulipokuwa tunaongea nae, tunachange namba, tukamwambia sisi tunatokea Africa, akesema, “Iwish to be in Africa”, nikamwelezea huyu ni msanii wangu mkubwa, baada ya kuangalia profile ya Diamond akawaka vile. Haijaishia hapo tukabadilishana na namba, na mchizi anatamani kuja hata Bongo anytime. Tunachat nae kidogo, soon tunaenda Marekani kuna kitu tunaenda kufanya najua tutakutana nae na tutamaliza maongezi yetu, hauwezi jua labda Diamonds are Forever inayokuja mwaka huu tunawweza tukamwalika”, alisema BabuTale.
Chanzo:Bongo5




Leave your comment