TANZANIA: Mr Blue apata menejimenti mpya kutoka Afrika Kusini.

 

 

Msanii wa muziki nchini Tanzania, Kherry Sameer Rajab a.k.a Mr Blue amedai kuwa amepata menejimenti mpya kutoka Afrika Kusini na ndiyo itakayomsimamia kazi zake.

Akizungumza  katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm, msanii huyo ammesema kwa sasa yuko na menejimenti mpya na wameshamtafutia kolabo na msanii mkubwa wa Afrika. “Kwakweli mwaka huku nashukuru nimeunza vizuri kwangu kwasababu kwanza nimepata menejimenti nzuri sana ambayo ipo ‘South Africa’, jamaa ni watanzania wanaoishi kule wameuona muziki wangu ni mzuri sema nimekosa ‘Kampani’ ya watu wakunisapoti kwahiyo wamejitolea kunisaidia na mwaka huuu nitafanya video kubwa na msanii mkubwa Afrika”, alisema Mr. Blue.

“Kwahiyo Mungu akinisaidia mwaka huu nitafanya video kubwa na msanii mkubwa Africa  ambaye siaki kumtaja mapema. Kwahiyo wimbo utaandaliwa Afrika Kusini pamoja na video japokuwa kuna nyimbo kadhaa nimeshazirekodi nitazitoa kwanza halafu hiyo ya kimataifa itatoka katikati ya mwaka huu au mwishoni”, aliongeza Mr.Blue.

 

Chanzo: Bongo5

 

 

 

 

Leave your comment