TANZANIA: Sifikirii kufanya kolabo na msanii wa nje kwa sasa – Mwana Fa

 

 

Mwana Fa anasema imefika wakati muziki wa Nigeria unaabudiwa hapa Tanzania lakini yeye anaamini nyimbo zao ni takataka. Akiongea jana kwenye kipindi cha ladha 3600 cha EFM , ndiyo maana wasanii wengi wanaposema wanataka kufanya kolabo ya kimataifa humaanisha kolabo ya kinigeria.

Aliongeza kuwa ndiyo maana yeye hana mpango wa kufanya kolabo yoyote na msanii wa nje kwa sasa, hasa kutoka nchini humo. “Muziki ninaoufanya ni kwa ajili ya watu wa hapa, mimi nauza mashairi, lugha ninayoitumia na presentation ninayoifanya na jinsi watu wanataka warelate na muziki wangu ni mazingira yanayonizunguka mimi moja kwa moja. Kwahiyo kama collaboration zitakuja zije, nikitaka kufanya na wasanii wa nje wala si kitu kigumu kabisa lakini si kitu ninachokifikiria sana sababu sio direction ya muziki wangu ninaotaka kuipeleka” aliongeza Fa.

 

Chanzo: Bongo5

 

 

 

Leave your comment