TANZANIA: Ne-Yo kutumbuiza nchini Tanzania jijini Mwanza, May 5!
18 February 2016

Msanii wa muziki wa Marekani, Shaffer Chimere Smith maarufu kama Ne-Yo anatarajia kutumbuiza jijini Mwanza May 21 mwaka huu.
Mwanamuziki huyo atatumbuiza katika tamasha kubwa la kila mwaka la Jembeka linalotayarishwa na kituo cha redio cha Jembe FM cha jijini humo.
Kwa msanii huyo hii itakuwa ni mara ya tatu kuja Afrika Mashariki. Ameshatembelea Kenya alikoenda kwenye Coke Studio Afrika mwaka jana na Uganda kwa ajili ya kutumbuiza.
Ndani ya tamasha la Jembeka pia Diamond ambaye mwaka jana walifanya kolabo na Ne-Yo atakuwepo.
Kituo hicho cha redio kinachofanya vizuri jijini Mwanza, hivi karibuni kiliwaleta wasanii kutoka Nigeria, Seyi Shay na Tekno kwenye tamasha la utangulizi Muzika lililofanya vizuri.




Leave your comment