TANZANIA: Nimegundua siri itakayonirudisha kwenye chati – Jaffarai

 

Mwanamuziki Jaffarai amesema amegundua siri itakayomrudisha kwa haraka zaidi kwenye muziki.

Akiongea na mtangazaji wa Hits FM ya Zanzibar D’ Swagga, rapper huyo ambaye pia ni mjasiriamali amesema, “Kwa sasa ni kuisoma tu game, wasanii wengi wakongwe wanafeli kwasababu hawafanyi muziki wa sasa wakati mashabiki wamebadilika, mashabikia wanataka muziki wa kucheza”.

“Mipango ni mingi na biashara yangu inanikwamisha kutoa wimbo mpya”, aliongeza.

Pia msanii huyo amedai hivi karibuni ataachia wimbo mpya.

Leave your comment