EXCLUSIVE (TANZANIA) – Msechu kufungua milango kwa yeyote kumwandikia nyimbo

Peter Msechu ni miongoni mwa wasanii wachache ambao hawaoni shida kukiri kuwa si wazuri kwenye upande wa uandishi wa nyimbo, licha ya kuwa na kipaji cha kuimba na kucheza vyombo vya muziki.

Baadhi ya wasanii (Tanzania) hawapendi kusema ukweli pale wanapoandikiwa nyimbo na watu wengine, wakidhani watu wakijua wameandikiwa inaweza kuwapunguzia thamani.

Msechu ambaye ametoa wimbo mpya wiki iliyopita amesema kuwa baada ya kugundua kuwa sio mzuri katika upande wa uandishi wa nyimbo, sasa hivi nyimbo zote anazorekodi atakuwa anawapa watu wengine kazi ya kuandika na kumpa njia na sauti ya kuimbia (melody).

“Unajua nimekuja kujua kuwa nilikuwa sijitambui nilikua nalazimisha kuandika nyimbo kitu ambacho nilikuja kugundua kuwa mimi sio mzuri upande huo”. Alisema Peter kupitia Amplifaya ya Clouds Fm.

Msechu alisema wimbo wake wa ‘Nyota’ ambao wote aliandikiwa na Amini ndio umetokea kuwa wimbo mkubwa na uliompa mafanikio kuliko nyimbo zote alizowahi kufanya.

‘Nyota’ ndio wimbo ambao pia ulimpa nafasi Msechu ya kutajwa kuwania tuzo za kimataifa AFRIMA 2014 za Nigeria kwa mara ya kwanza. Ambapo pia wimbo alioutambulisha wiki iliyopita wa ‘Malava’ umeandikwa na Barnaba. Msechu amefungua milango kwa msanii au mwandishi yeyote anayehitaji kumwandikia nyimbo na yupo tayari kufanya naye kazi.

Leave your comment