EXCLUSIVE (TANZANIA) – Mo Music kwenda kushoot video ya ‘Skendo’ nchini Afrika Kusini
1 December 2015

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Moshi Katemi aka Mo Music anatarajia kwenda Afrika Kusini kushoot video ya wimbo wake alioutoa hivi karibuni wa ‘Skendo’.
Msanii huyo amesema licha ya kwenda kushoot nje bado atamtumia director wa hapa nyumbani Adam Juma, ambaye ndiye aliyeshoot naye video zake mbili zilizopita.
“Sitaki kuwaangusha mashabiki wangu, nitakwenda Afrika Kusini kufanya video ya Skendo ila nitamtumia Adam Juma kwasababu ni mwongozaji bora na huwa tunafanya kazi nzuri tunapokutana”, alisema Mo Music.
Source: Mtanzania




Leave your comment