EXCLUSIVE (TANZANIA) – Jay Mo ataachia wimbo mpya wa ‘Hili Game’ ijumaa ya leo
27 November 2015

Msanii Jay Mo aliyekuwa kimya kwa kipindi kirefu sana, ijumaa ya leo ataachia wimbo mpya uitwao ‘Hili Game’. Wimbo huo utakuwa wa kwanza kuutoa tangu mara ya mwisho alipoachia wimbo miaka mine iliyopita.
Akizungumza na 255 ya XXL ya Clouds FM, Jay Mo alisema wimbo huo umetayarishwa na P Funk majani.
“Mungu akipenda ijumaa itakuwa birthday tunaweza tukaachia wimbo wa kwanza Jay Mo baada ya miaka 4” alisema Jay Mo.
“Wimbo unaitwa ‘Hili Game’ na utakuwa muda mzuri kwasababu nimeelezea muziki ulipotokea mpaka ulipo sasa. Zamani ilivyokuwa na ugumu wake. Kwahiyo vitu kama hivyo vitakuwa ni elimu nzuri kwa hawa wasanii wa katikati ambao hawakujua tulipotokea”, aliongeza.
“Plan yetu tunataka Disemba tena kabla ya mwaka mpya tutoe nyingine. Kuna ngoma kama tano ambazo zipo tayari lakini ilikuwa baada ya ukimya sana Jay Mo hawezi kurudi na bonge moja la track. Nikaona bora nianze pale nilipoishia halafu baada ya hapo tukae mkao wa kula vitu vikali vitakuja. Tunaonekana kama hatupo kumbe tupo na uwepo wetu ni mkubwa”, alimzalizia Jay Mo.




Leave your comment