EXCLUSIVE (TANZANIA): Navy Kenzo Watangaza Collabo Na Kundi Hili La Muziki Kutoka Ghana!


Good news kwako shabiki wa muziki wa Bongo Fleva, kundi la Navy Kenzo linaloundwa na Producer Nahreel na mpenzi wake Aika limeshare na sisi kupitia page yao ya Instagram ujio wa collabo mpya na kundi la muziki kutoka Ghana, R2bees!


Kupitia official Instagram page ya kundi la Navy Kenzo @navykenzoofficial, wamepost picha na caption inayosema…

Kundi la R2bees kutoka Ghana linaundwa na ndugu wawili, Faisal Hakeem maarufu kama Paedae da Pralem na Rashid Mugeez maarufu kama Mugeez… kundi hilo pia limeshawahi kunyakuwa tuzo kubwa za kimataifa ikiwemo BET Awards 2013 ‘Best International Act: Africa na kwa upande wa tuzo za nyumbani, R2bees wanashikilia tuzo 9 za Ghana Music Awards.

Navy Kenzo walikuwa Johannesburg, South Africa kwa ajili ya kuperform kwenye tamasha la African Music Concert maarufu kama AMC 2015, na baadhi ya wasanii waliohudhuria tamasha hilo ni pamoja na mtu wetu Vanessa Mdee,Wizkid, Davido, AKA, Victoria Kimani, Runtown na wengine kibao.

Leave your comment