VIDEO OF THE DAY (TANZANIA): Video Inayoongelewa Zaidi Wakati Huu Kutoka Kwake Shaa!


Baada ya MTV Base kufanya exlcusive premier mwimbaji Malkia wa Uswazi Tanzania Shaa ameweka video yake mpya kwenye Youtube kwa ajili ya mashabiki wake dunia nzima kuona chake kipya kwenye headlines sasa hivi.

https://www.youtube.com/watch?v=fs7l2IfXDCo
Baada ya kuiona video yenyewe, haya ni mambo sita ambayo unatakiwa kuyajua kwenye hizi headlines mpya za Shaa kwenye nukuu.

1) ‘Audio ya Toba nimerekodi miaka 2 iliyopita na video yake nime-shoot mwaka jana ila tu imechelewa kutoka na ratiba mbalimbali kwenye kazi zangu nyingine’

2) ‘Producer wa hii beat anaitwa Big H ambae ni Mnigeria tulikutana tu kwenye mitandao, alisema anapenda kazi zangu na mimi nikamwambia napenda kujua kazi zake, akanipa beats mbalimbali nikapenda hii ya Toba ndio nikatumia kama hivi.

3) ‘Kwenye shooting pale mnavyoona tunacheza na mikono kama kundi flani hivi la kihindi tulijifunza palepale location, kuna style moja ambayo director alisema haipati vizuri kwenye camera, so akasema hamna style nyingine yoyote ndio tukafanya ile palepale na ikatoka poa kama inavyoonekana’

4) ‘Hii video kuna dancers raia wa nchi mbalimbali, kuna dancer raia wa South Africa, Mholanzi, Mchina na wengine kwasababu ya kile kikundi cha dancers nilichopata tofauti na video zangu nyingine natumiaga dancer wa hapahapa home’

5) ‘Hii ndio video yangu ya kwanza kuitoa official nikiwa nimefanya na director Justin Campos ambae ame-shoot video na Vanessa Mdee, Jux , Joh Makini, Ben Pol na wengine’

6)Pia ilibidi video hii ifanywe na directors wawili ambao ni Adam Juma na Justin Campos mwenyewe lakini kutokana na ratiba kutofautiana ikashindikana Adam kushiriki akafanya Justin mwenyewe.

Source: Millardayo

RELATED 

 EXCLUSIVE (TANZANIA): Msami Baby Kufanya Ngoma Na Mkali Wa Nigeria, Tekno!

Leave your comment