EXCLUSIVE (TANZANIA) – Mayunga tayari awasili Marekani katika Stusio za Universal
20 November 2015

Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Star, Mayunga ameonesha furaha yake baada ya kufika kwa mara ya kwanza kwenye studio za Universal Studios, Hollywood nchini Marekani.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram alipost picha na kuandika;
“Kwa mara ya kwanza ndani ya UNIVERSAL STUDIOS…. HOLLYWOOD OOW asante sana Mungu asante sana @Airtel Trace music star pia asante sana watu wangu wazuri. Unajua nini usiache mtu yoyote akusimamishie ndoto zako kwasababu nilikua na ndoto kwamba siku moja ningependa kuwa UNIVERSAL STUDIO. . HOLLYWOOD OOW siwezi hata kuelezea sana kwani ni zaidi ya furaha, ninachoweza sema ni kwamba ungana nami katika safari hii ili tuweze kushea baadhi ya vitu nawapenda sana sante”.
Mayunga alipata nafasi hiyo kwa kushiriki shindano la Airtel Trace Music Star, na moja ya zawadi ilikuwa ni kwenda kuonana na Akon katika studio zake huko Marekani.




Leave your comment