EXCLUSIVE (TANZANIA) – Shaa kuachia video ya Toba iliyoongozwa na Justin Campos hivi karibuni.

 

Wasanii kwa sasa hushoot video na kukaa nazo bila kuziachia wala kusema chochote. Kati ya wasanii hao mwanadada Shaa ni mmoja wao, ukimya wake haumaanishi hakuna vitu vikubwa vinavyoendelea kufanyika.

Muimbaji huyo miezi kadhaa iliyopita alisafiri hadi Afrika Kusini kwenda kushoot video ya wimbo wake kwa muongozaji pendwa Afrika, Justine Campos.

Mke wa Justine, Candice alipost picha  ya screen shot kwenye Instagram kile kinachoonekana ni video ya wimbo uitwao Toba na kuandika: "Something Awesome coming !!! @shaa_tz @masterjtz”.

Picha hiyo ikimuonesha Shaa akiwa amepaka hina katika sehemu zake za mwili, ambapo pia Shaa mwenyewe amepost picha kama hizo katika Instagram yake bila kuandika chochote.

Leave your comment