EXCLUSIVE (TANZANIA)- Leyla (Fairy Voice)- aliyeshinda shindano la Yemi Yalade kwa Cover.

 

 

 

 

Msanii chipukizi Leila a.k.a The Fairy Voice maarufu kwa kuimba nyimbo za wasanii wengine yaani Cover, hivi karibuni ametoa wimbo wake unaoitwa ‘Hoi Hoi’. Msichana huyo ambaye ni mwenyeji wa Mwanza anayeishi Dar es salaam kimasomo amejipatia umaarufu katika mtandao wa kijamii wa Istagram kwa kufanya cover.

“Napenda sana kuimba nyimbo za watu na kupost kwenye Instagram yangu” Layla alikiambia kipindi cha The Bridge cha Radio Free Africa, Jumapili ya Novemba 15.

“So hiyo ilinijengea nikimuimbia mtu nyimbo yake nafurahia, ilinijengea umaarufu na wasanii wengi ndani nan je ya nchi” aliongeza Layla.

Kupitia umaarufu wake wa Instagram aliweza kushiriki shindano lililoandaliwa na muimbaji wa Nigeria, Yemi Alade. Zawadi ya iPhone 6 na kula dinner pamoja na Yemi.

“Unfortunately mpaka leo bado sijapata but it’s okey” alisema Layla.

Leyla aliongeza kuwa anaelewa kuwa Yemi anaweza kuwa amekumbwa na mambo mengi ila amefurahi kwa kuweza kushiriki na imempa promo kubwa sana.

Pia aliweza kurekodi wimbo wake mpya wa ‘Hoi Hoi’ kwa Manecky aliyemfahamu kupitia mdogo wa mtayarishaji huyo wa muziki.

Leave your comment