EXCLUSIVE (TANZANIA)- Vanessa na Diamond washinda tuzo 4 za AFRIMA Nigeria

 

 

 

Hivi karibuni tuzo za All Afrika Music Awards 2015 (AFRIMA) zilizofanyika jumapili ya tarehe 15 mwezi huu jijini Lagos, Nigeria. Ambapo Tanzania imetoa washindi wawili yaani Vanessa Mdee na Diamond Platnumz.

Vanessa ameshinda katika kipengele cha ‘Best African Pop’ kupitia wimbo wake wa ‘Hawajui’. Kupitia ukurasa wake wa isntagram Vannessa aliandika,

“GLORY TO GOD IN THE HIGHEST! #Hawajui thankyou@nahreel @barnabaclassic and #Tanzania #Africa for letting me sing my song, this one is for you !!

Kwa upande wa Diamond ambaye ameshinda vipengele vitatu, ikiwemo kipengele cha Msanii Bora wa Mwaka (Artist Of The Year) ambapo ilikuwa ikiwaniwa na Ali Kiba, Davido, Jose Chameleone, Wizkid, Yemi Yalade, Sarkodie na Flavour.

Vipengele vingine alivyoshinda ni Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki (Best Male Artists in Eastern Africa) pamoja na wimbo bora Afrika (Nasema Nawe).

Msanii mwingine wa Tanzania aliyekuwa akiwania tuzo hizo ni Linah katika kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki, lakini hakubahatika kushinda kipengelehicho.

Leave your comment