EXCLUSIVE (TANZANIA)- Mo Music kusherekea siku ya kuzaliwa kwa kuachia wimbo mpya Nov 14.

 

 

 

Mwaka jana msanii Mo music alikosha nyoyo za wapenzi wa Bongo Fleva kwa wimbo wake wa ‘Basi Nenda’ ambao ulikubalika sana na kusikika kila mahali. Mo Music anakuja tena na single mpya iitwayo ‘Skendo’.

Nyimbo hiyo itakayotoka Novemba 14 ikiwa pia ni siku ya kuzaliwa ya Mo Music ambaye jina lake halisi ni Moshi Mtui kutoka Mwanza. Amechagua nyimbo yake hiyo  ya ‘Skendo’ baada ya ‘Nitazoea’ kutoka katika siku hiyo maalum ya kuzaliwa kwake.

Nyimbo ya Skendo imeandikwa na kutayarishwa na Lollypop ambaye pia ndiye alieandika wimbo wake wa ‘Basi Nenda’.

Pia hivi karibuni Mo Music alisema kuwa yeye na management yake wana mazungumzo na mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ awe video model kwenye video yake mpya.

Source:Bongo5

Leave your comment