EXCLUSIVE (TANZANIA)- Sio kila msanii wa nje ni wa kufanya naye kolabo – Joh Makini

 

 

Msanii Joh Makini ametoka kuitambulisha video mpya ya ‘Don’t Bother’ aliyoshirikiana na AKA toka Afrika Kusini Novemba, 10 jana katika kituo cha runinga cha MTV Base.

Kutokana na kolabo hiyo ni wazi kuwa wawili hao wataongeza mashabiki kutokana na kwamba wote ni wasanii wakubwa katika nchi zao, lakini Joh Makini ametoa mtazamo wake wa kolabo kama hizo kama watu wanvyofikiria ndio vigezo vya ukubwa wa msanii.

Kupitia XXL 255 ya CloudsFM Joh Makini alisema “Tumeshafanya kazi na watu wengi lakini unajua pia sio lazima sana sisi kufanya kolabo na wasanii wa  nje  ndio tuonekane sisi wakubwa”. Pia akatolea mfano wa wimbo wake uliopita wa ‘Nusu Nusu’ ambayo hajamshirikisha msanii yoyote kutoka nje zaidi ya G Nako.

 ‘…kwasababu 'Nusu Nusu' sina msanii wa nje mle ndani na ngoma inafanya vizuri, kwahiyo sio kila msanii wa nje tutampapatikia kufanya nae kolabo, inategemea na feeling na aina ya msanii mwenyewe”

Wimbo huo wa 'Nusu Nusu' ulifanyiwa video na Justin Campos huko Afrika Kusini na imeshika chati mbalimbali ya vituo vikubwa vya runinga Afrika.

Leave your comment