EXCLUSIVE (TANZANIA)- Navy Kenzo kuchaguliwa kuwania tuzo za ‘Top Naija Music Awards 2015’ za Nigeria

 

 

Kundi la Navy Kenzo lachaguliwa kuwania tuzo za ‘Top Naija Music Awards 2015’ za Nigeria. Katika kipengele hicho kundi hilo linawania na makundi mengine ya Nigeria ambayo ni Dupi 2, Connect Music Group (CMG), Ace Republic, Dp-Kings na Betrose.

 Kura za shindano hilo zimeanza kupigwa tangu Novemba 8, 2015 na zitafungwa Disemba 31,2015 na washindi wa tuzo hizo watatangazwa Januari, 2016 huko jijini Lagos, Nigeria.

Navy Kenzo wametoa taarifa hizo kupitia ukurasa wao wa Instagram;

“Kundi bora la muziki toka #+255 Navy Kenzo lachaguliwa kuwania kipengele cha #KundiBoraLaMuzikiAwards katika tuzo za #TopNaijaMusicAwards za nchini Nigeria …uwanjawa kupiga kura umeshafunguliwa kura yako ni muhimu sana kwetu tunaomba ushirikiano wako. LINK YA KUPIGIA KURA IPO KWA BIO YETU..

#AboveInAMinute #GameGame #ThankYouGuys #VoteVoteVoteForUs   

Leave your comment