EXCLUSIVE (TANZANIA)- Sababu iliyowapeleka Young Dee na Nyandu Tozi Afrika Kusini
6 November 2015

Katika mtandao wa kijamii wa Instagram hivi karibuni account za Young Dee na Nyandu Tozi zimekuwa zikiwaonyesha wasanii hao wakiwa nchini Afrika Kusini na hawakuweka wazi walikuwa huko kwa shughuli gani. Wengi walihisi kutokana na wasanii wengi kwenda nchini humo kufanya video wakahisi nao pia wameenda kwa shughuli hiyo.
Young Dee na Nyandu Tozi wamesema wapo Afrika Kusini kufanya show. “Nipo hapa na Nyandu Tozi maeneo ya Johanersburg kwa ajili ya maandalizi ya show yetu ambayo tutaifanya pale Pretoria tarehe 7 jumamosi mwezi huu wa 11” Young D aliiambia 255 ya Clouds FM.
“Kikubwa ni hicho ndo kimetuleta huku kwasababu tumeamua kufunga mwaka kwa style tofauti kidogo kwasababu sehemu kubwa ya Tanzania tumeshaimaliza na tukaona kuna mashabiki zetu wengi sana huku ambao hawajawahi kuniona na hawajawahi kupata bahati ya kuona performance yangu’. Alisema Young D.
Mbali na show hiyo kuna kitu kingine ambacho kimewapeleka; “ Na ukiachia hivyo kuna mipango mingine kibao ambayo tutawapa taarifa as long as mtakuwa karibu na sisi na tutawajulisha, kingine ambacho kitatokea pande hizi” alimaliza Young Daresalaam.




Leave your comment