EXCLUSIVE (TANZANIA)- Papa Wemba ndani ya Karibu Music Festival leo- Bagamoyo

 

Baada ya kusubiri kwa muda mrefu tamasha la muziki la Karibu Music Festival linaanza leo tarehe 6 hadi 8 jumapili, watakuwepo wasanii wa ndani na kutoka nje ya nchi. Linalofanyika katika viwanja vya Mwanakalenge huko Bagamoyo.

Kati ya mastaa wanaohudhuria tamasha hilo ni Papa Wemba kutoka Kongo atakaejumuika na wasanii /vikundi zaidi ya 30 katika steji.

Papa Wemba ni mwanamuziki nguli na mwenye mashabiki duniani kote, alianza muziki miaka ya 1960, muziki wake una mahadhi ya kiasilia, kimataifa na wenye mvuto. Kati ya nyimbo zake ni Bravo Cathy, Yolele,Maria Valencia, Show Me The way na nyingine nyingi.

Tamasha la Karibu Music Festival mwaka jana liliuza zaidi ya tiketi 12,000 na waandaji wa tamasha hilo wanakadiria namba ya mwaka huu kuongezeka hadi 15,000 hadi itakapofikia msimu wa pili wa bonanza hilo.

Tiketi zinapatikana mlangoni au unaweza kutoa oda kabla kama inavyoonekana kwenye picha.

Source: The Citizen

Leave your comment