EXCLUSIVE (TANZANIA)- Sitaoa kuwaridhisha watu-Izzo Bizness
6 November 2015

Rapper wa muziki Tanzania Izzo Bizness anaeiwakilisha Mbeya city amesema hawezi kuoa ili tu kuwaridhisha watu japo yupo katika mahusiano na ingawa ndoa jambo la lazima. Tumewasikia mastaa wengi wakitoa sababu za kuyokuoa au kuolewa kwa sasa, na hii ndiyo sababu ya Izzo B.
Kupitia Planet Bongo ya East Afrika Radio alisema “Umri unaenda lakini ndoa ni mipango, siwezi kuoa ili kuwaridhisha watu kwa kuwa mimi ni kioo cha jamii, si kitu rahisi kama watu wanavyofikiria ingawa niko kwenye mahusiano”
Pia aliongeza kuwa hapendi mtoto wake apitie maisha aliyopitia yeye hivyo anajipa muda wa kujipanga vizuri kumtafutia maisha.
“Nina mtoto mmoja anaitwa Pauline nampenda sana, sihitaji aje ku-experience vitu ambavyo mimi nimepitia, lazima nimtengenezee future, lazima nihakikishe ataenda shule nzuri,atapata elimu bora na tunafahamu gharama za watoto kuhusu shule. Kwahiyo nina muda mwingi sana wa kukaa na kupanga kwanza maisha ya mtoto ingawa ndoa ni lazima lakini kwa sasa ni mapema sana kuzungumzia” Izzo alimaliza kwa kusema hayo.




Leave your comment