Women Crush Wednesday (WCW)- Urembo, mahusiano na kung'ara katika tasnia ya muziki - Linah

 

Mwimbaji na mwigizaji aliyeanzia katika nyumba ya sanaa ya Tanzania House of Talent (THT ) Linah Sanga, mwanadada huyo anaytamba na kibao chake 'No Stress'. Msanii huyo ambaye aliigiza katika tamthiliya ya 69 records, kwa zaidi ya miaka minne alikuwa chini ya management ya THT na hatimaye baadae kutoka katika uongozi huo.

Baada ya kutokaTHT akawa chini ya NFZ (No Fake Zone), baada ya NFZ alipata deal na kusign na Pana Music. Mwanadada huyo alianza kutamba na kibao cha Atatamani na kufuatia na nyimbo nyingine nzuri. Ila kwa sasa anatamba na "ole Themba" , No Stress na hivi karibuni alisema anatarajia kutoa wimbo mpya unaitwa Happy Day,

Pia Linah ameweza kupambana na changamoto za kimaisha kama mahusiano, kuendeleza career yake na kubaki kuwa mrembo.Katika maisha ya kawaida kuna break up na make ups,Linah alikuwa mpenzi wa Amini na baadae kuachana lakini hiyo haikumfanya kushindwa kuendelea mbele. Hivi sasa mwimbaji huyo amechaguliwa kuwania tuzo za AFRIMMA katika kipengele cha Best Female Artists in East Africa (Best Artist in African Contemporary).

Zaidi kila lakheri katika kupambana na kujitafutia riziki, na hongera kwa kuufanya muziki wa Tanzania kuendelea kuwa kileleni na kuitambulisha nchi ya Tanzania na asili yake.

Leave your comment