EXCLUSIVE (TANZANIA)-Linah akanusha habari ya kuwa na ujauzito
4 November 2015

Linah Sanga akanusha kuwa na ujauzito na kutoa taarifa kuwa yuko sawa katika suala la uzazi.
Mwimbaji huyo wa ‘No Stress na Ole Themba’ amesema kwa sasa anajipanga na ndio maana hajaamua kupata mtoto, hivyo hiyo haimaanishi kuwa ana tatizo la uzazi kama watu wengi wanavyosema.
“Mimi nipo vizuri bhanaa sina tatizo la uzazi ila hua najipanga ndio maana watu hawajawahi kuniona nina ujauzito, lakini kwa sasa najiachia Sanaa hivyo muda wowote wanaweza kusikia jambo”, alisema Linah kupitia Planet Bongo ya EATV.
Kwa msanii huyo si mara ya kwanza kukanusha taarifa za kuwa mjamzito. Mwaka jana 2014 mwanzoni Linah aliwahi kukanusha taarifa kama hizo na kusema maswala ya ujauzito, kuolewa na kuwa na familia ni ya muhimu kwa kila msichana ila kwa yeye ulikuwa muda haujafika bado.




Leave your comment