EXCLUSIVE (TANZANIA)- Baada ya kushoot video Afrika Kusini sasa ni kolabo na Mafikizolo- Chege
3 November 2015

Msanii wa Bongo Fleva yupo Afrika Kusini kipindi hiki kushoot video mpya iitwayo Sweety sweety aliyomshirikisha Runtown na msanii mwingine toka kundi la Uhuru.
Habari njema zaidi ni kwamba Chege Chigunda ana mpango wa kufanya kazi na Mafikizolo wa Afrika Kusini ambao ni mastaa wa nyimbo inayotamba ya ‘Khona’ waliochukua tuzo mbili za MTV 2014.
Kwa mujibu wa blog ya Millardayo.com Julio Batalia ambaye yuko na Chege na Mafikizolo, amesema tuombeane kheri ili tufanye kitu kizuri ambacho kitapendeza na kuiwakilisja Tanzania. Tuendelee kupeana support na tufanye mambo makubwa’.




Leave your comment