EXCLUSIVE (TANZANIA)- Ommy Dimpoz kurekodi na Eddy Kenzo baada ya kushinda tuzo Marekani
2 November 2015

Pichani:Ommy Dimpoz, Mubenga na DMK -Wakiwa RedCarpet.
Ommy Dimpoz ameshinda tuzo za African Entertainment Awards zilizofanyika jumamosi hii huko New Jersey, Marekani.
Ommy alishinda katika kipengele cha People’s Choice Award na pia alitumbuiza katika tuzo hizo.
Kutokana na ushindi huo Ommy Dimpoz aliandika kupitia ukurasa wake wa Instagram, “Thank you my people for your Votes U made this This Possible #PeopleChoiceAward @africanentertainmentawards#NewmusicComingSoon”. Waandaaji wa tuzo hizo mpaka jumapili walikuwa hawajatangaza orodha kamili kamili ya washindi.
Pia msanii huyo anayetamba na kibao cha Wanjera na muimbaji wa Uganda Eddy Kenzo, wameingia studio na kurekodi wimbo pamoja.
Dimpoz aliweka kipande cha video kwenye instagram kinachowaonesha Kenzo akiingiza sauti za wimbo huo huku Dimpoz akisikika akimpa maelekezo kadhaa ya kuboresha vionjo vya wimbo.
Wawili hao walikutana Marekani walikoenda kuhudhuria tuzo hizo ambapo Eddy naye alalishinda.




Leave your comment