EXCLUSIVE (TANZANIA)- “Game” ya Navy Kenzo na Vanessa Mdee kufika nafasi ya juu kwenye Chat ya Trace-Nigeria
2 November 2015

Wasanii wa Tanzania wameendelea kuitangaza vyema nchi yetu ya Tanzania kutokana na muziki wake kushika nafasi za juu kimataifa. Kundi la Navy Kenzo wameshika nafasi ya juu katika chat ya Trace Nigeria na video yao ya “Game” waliyomshirikisha Vanessa Mdee kwa kuwa namba 1 kwenye chati ya African Chati. Hapo awali tarehe 30 Septemba 2015 wimbo huu ulifanikiwa kushika namba 1 kwenye chati ya MTV Base Official African Chart ya Afrika Kusini.
Muziki wa Tanzania unashika kasi na kutamba katika chaneli za kimataifa kama Trace, MTV Base na kufanya Tanzania kujulikana zaidi. Pongezi ziende kwa Navy Kenzo na Vanessa Mdee kwa kazi nzuri.




Leave your comment